elizabeth ndani ya mjengoni leo jioni
Thursday, November 12, 2009
Hata mimi nilipata wasaa angalau wa kumpa hongera mshiriki wetu Elizabeth aliyetoka kwenye shindano la Big Brother Africa Revolution.
Elizabeth akimpa saluti ya kutosha kabisa Kapt. Gadna G Habash mara baada ya kumaliza kipindi chake cha Jahazi leo jioni kupitia redio ya Clouds FM.
Elizabeth akijibu moja ya swali aliloulizwa na mtangazaji wa Choice FM, ML Chris kuhusiana ushiriki wake katika shindano la Big Brother Africa Revolution leo jioni.
Pichani ni aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta alipokuwa akifanya mahojiano na Ml Chris leo jioni kupitia redio ya Choice FM,iliopo Mikocheni jijini Dar.
Pichani ni Aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta alipokuwa akifanya mahojiano Kapt Gadna G Habash kupitia kipindi cha Jahazi leo jioni kinachorushwa na redio ya Clouds Fm 88.4,shoto ni Meneja Huduma wa Multchoice Ronald Shelukindo aliyekuwa ameambatana nae.Elizabeth amesema kuwa kwa ana mpango wa kuendelea na masomo,lakini kwa sasa anataka ajishughulishe zaidi katika mambo ya burudani ikiwemo suala la uigizaji filamu,utangazaji na mambo mengineo yanayohusiana na nyanja hiyo kwa ajili ya kujipatia kipato zaidi ili aweze kuendelea na masomo,aidha Elizabeth amesema kuwa atashukuru sana kama atajitokeza mfadhili wa kumpa sapoti katika kakamilisha safari yake ya mosomo.Eliza a,emeongeza kuwa yeye tayari ana mchumba ambaye yuko ughaibuni mambo yakiwa tayari basi kila mmoja atamfahamu.
Maoni: 4
« Rudi Mwanzo | Post a Comment
Jr Mchumba amsomeshe,asitafute mfadhili!
MHH HIYO SERO DISTANCE JAMANI WE EBU ACHA HIZO!!
We GADNA taratibu hapo!
Mambo hayo tuachie wenyewe.
Mambo hayo tuachie wenyewe.
Mkuu mambo yako sio mabaya ingekuwa ni usiku wa pekecha pekecha ningesema ukiondoka hapo ukakoge any way all the best unafanya mazuri zaidi kwa jamii kuliko mabaya thank for that.


