pumzika kwa amani michael jackson

Wednesday, July 8, 2009
Kwa wale ambao hawakuweza kushuhudia utoaji wa heshima za mwisho kwa Marehemu Michael Jackson kupitia vyombo mbalimbali vya Luninga ikiwepo TBC1 hivi ndivyo mambo yalivyokuwa kwa ufupi katika ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles Marekani ambapo zaidi ya watu 80.000 walihudhuria utoaji waheshima za mwisho wakiwemo watu maarufu mablimbali katika picha kama unavyoona, ni ndugu wa Marehemu Michael Jackson wakitoaJ eneza la Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jackson ,mwanamuziki huyo alifariki juni 25 nchini marekani na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa anatarajiwa kuzikwa leo mara baada ya mwili wake kuagwa rasmi jana (picha kwa hisani ya mtandao).

Dada wa marehemu marehemu Michael Jackosn, Jannet Jackson akiwa na watoto wa marehemu, kulia Catherine na Paris na ndugu zao wengine.

Ndugu na jamaa wa Marehemu Michael Jackson wakiwa wamekaa wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Michael Jackson kabla ya mazishi.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 08, 2009 | | Permalink |

Maoni: 1

  Tarehe July 8, 2009 8:29 PM Anonymous Anonymous Anasema:
FYI - MJ ALIKUWA NA MTOTO WA KIKE MMOJA TU.......Paris Katherine.


Idadi ya watu