mie mjumbe tu wa haya wanajamvini

Thursday, July 9, 2009
Mambo vipi kaka?

Hongera sana kwa kazi nzuri sana naomba unitolee hii ili nipate mawazo ya wadau wengine.

Nimesikia sana libeneke la VISACARDS za crdb kuwa unaweza kuzitumia online lakini kuna mdau mmoja anasema ni hatari sana pale unapojaza hizo form ukiweka tu zile no nyuma ya card mtu ana uwezo kwa kudraw visenti vyako vyote,sasa mimi nataka kujua wanadraw vipi na mtu utajuaje kuwa hii ni kampuni halali na hii ni fake?
Na kuna jingine mi linanisikitisha sana khusu hii bank ya CRDB yaani ukidraw pesa tu wanakukata sh 400 sasa kwa mfano kwa mwezi ukidraw pesa labda mara 20 almost elfkumi,
Sasa mi najiuliza hivi hii bank kumbe kila siku mtaji wake unakuwa kumbe kwa kutumia migongo ya sisi walala hoi na hiyo ni savings account,ya mimi mfanyakazi wa kima cha chini je mfanyabiashara au mtu unajenga na pesa yako iko hapo labda kila siku unadraw mara tano yaani kwa mwezi wanaingiza sijui billion ngapi?
Na hapo bado sijajua kuhusu hizo account nyingine naomba jamani mnijulishe na hasa hii account ya Malaika maana wanaitangaza sana.Mimi binafsi narudi bank yangu toka shule NMB ingawa nao network zao sijui za makete.
ASANTE SANA KAKA.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 09, 2009 | | Permalink |

Maoni: 5

  Tarehe July 9, 2009 10:59 AM Anonymous Anonymous Anasema:
mdau kuhusu swala la card usizungumze kabisa..
kuna kitu kinaitwa green card, one time nilicheza na nikatakiwa kulipia kiasi kadhaa cha fedha ( jamaa walikuwa wezi tu ) ingawa akaunti yangu ilikuwa nyeupe na nilikuwa sina mpango nayo, nikatoa namba za kadi na tarakimu nne za mwisho.

jamaa wanauwezo mkubwa wa kujua kuwa hii ni benki gani na inapatikana wapi.
wakaingia katika akaunti yangu na kutaka kudraw pesa... ikumbukwe kwamba akaunti yangu sio bongo, kwahiyo kulingana na security ya bank ninayotumia jamaa hawakuweza kuchukua pesa bila bank kunitaarifu.. so walinijulisha kuwa nimeruhusu pesa kutolewa, nikakataa na jamaa wakashindwa kuchukua. sijui kama bongo wanaweza kukutaarifu raia za kawaida... wanaweza kuacha masera wabebe tu mihera. hii inatokea hasa unapopoteza kadi.

Kwa hiyo ndugu yangu hilo linawezekana kabisa.
  Tarehe July 9, 2009 11:11 AM Anonymous Anonymous Anasema:
Kitu unachotakiwa kujua Buying Online ni Bonge La Risk,Kuna kitu kinaitwa "Hackers" Hackers ni watu wenye skills ya Juu kuhusu matumizi ya Computer so anaweza kuhack any transaction utafanya online.No matter uwe africa,Europe,Asia etc so wanauwezo wakuhack transaction yako ukiwasehemu yeyote.na wala siyo Bank yako.Ushauri wabure kama wewe ni mtu unaependa kufanya shopping online unatakiwa ktk account yako au card iwe atleast na the same amount ya kitu unabuy mfano unataka ununue kitu kinauzwa $300 basi acount yako inakuwa na $310 the same amount ya kitu unataka kununua.
  Tarehe July 9, 2009 12:39 PM Anonymous P Anasema:
Kama walivyosema wadau hapo juu, hii inategemea na security system ya bank au credit card unayotumia. Mi ninayo CRDB visacard na pia nina crediti card ya HSBC bank, naitumia sana hii ya nje maana security system yake iko juu, na sijawahi pata tatizo lolote la kuibiwa pesa, ila hata mimi naogopa sana kutumia ya home maana sielewi system yake ikoje. Kwa hiyo ndugu, kuwa mwangalifu sana wakati wa kutumia hiyo card yako, wajanja ni wengi na wanaishi kwa kazi hiyo ya kula kupitia migongo ya watu
  Tarehe July 11, 2009 2:33 PM Blogger ICT 255 Anasema:
Pitia Hapa

http://ict-tz.blogspot.com/2009/07/jiepushe-na-matumizi-yasiyo-halali-ya.html

Mdau nilishaelezea hili swala kirefu na njia za kujikinga kuathirika.

Tuko pamoja.
  Tarehe July 15, 2009 10:59 AM Anonymous Anonymous Anasema:
Mdau P hapo 12:39. haijalishi kama ni HSBC au la, ni kwamba ushukuru Mungu tu kwamba halijakukuta. Kuna mtu ali-hack-in kwenye akaunti za Langley (makao makuu ya CIA) na akavuta mkwanja!!! hivi security system ya HSBC ni kali kuliko ya CIA!!! Usitumie akaunti yenye bingo nyingi kununua Online. Wazee wa ebay mpoo??

Mdau chiggs, deslam


Idadi ya watu