huu ndio ujio mpya wa q-chila kwa sasa
Thursday, July 9, 2009

Mwanamziki mwenye sauti zenye kuwafanya watu waache kazi zao pale mziki wake wa Ubongo wenye akili yaani BONGO FLAVA Q Chief a.k.a Q Chilla kichwa chake sasa ni cheupe kama kiganja cha mkono kwa kuwa ameamua sasa rasta basi na kuonyoa nywele zake zote na kubaki na kialaza. Hivi sasa anatamba na kibao chake cha mnanda ambao pia unajulikana kama mchiriku.
Kuonesha upara huo unakwenda sambamba na mabadiliko yake makubwa katika fani ya muziki wa kizazi kipya,amejiunga ndani ya lebo ya studio za Bongo Records ilioko chini ya Prodyuza mahiri kabisa hapa bongo aitwaye P-Funk a.k.a Majani a.k.a Kinywele kimoja.
Sasa hivi bongo Records ina vichwa vipya kabisa,akiwemo Mangwear,Q-Chilla,C-Pwaa na wengine kibao,kama vile haitoshi ameongeza maprodyuza wengine wakali akiwemo Producer Q na Antonio.Baada ya hapo wadau wa muziki wa bongofleva kaeni mkao wa kula Jamvini.
Maoni: 1
« Rudi Mwanzo | Post a Comment
Amependeza sana,bora alivyo sasa kuliko ile mirasta.eeh kumbe yupo Handsome hivyo.


