alitangaza kustaafu mwaka 2002 na akarudi kwa kishindo mwaka 2004,kwanini ?

Thursday, July 9, 2009

Huwezi kuthubutu kuzungumzia muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava kama unavyojulikana kote ulimwenguni bila kumzungumzia na kumuhusisha moja kwa moja na muziki huo,Joseph Mbilinyi(pichani) ambaye kisanii tulianza kwa kumjua kama 2 Proud kabla hatujamuita Mr.II na baadaye Sugu.


Sugu sio tu alichangia kuipa Bongo Fleva utambulisho rasmi katika jamii,bali pia ni miongoni mwa wasanii “waasisi” walioamua kwa makusudi kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika kughani(rap) huku wakiwa na ujumbe ambao uligusa jamii inayowazunguka badala ya ile ya kusimuliwa au kuona katika luninga.Ukipenda unaweza kumwita “mwanamapinduzi”.


Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano.Katika mahojiano haya Sugu anabainisha mambo kibao yakiwemo masuala kama vile alipo na anachokifanya ,ushauri wake kwa wasanii wenzake katika masuala ya haki zao nk.Pia Sugu anajibu swali ambalo wengi wanaliogopa;je muziki wa bongo fleva uko katika njia sahihi?Kuna tofauti gani katika muziki huu tangu walipoanza na walipo hivi sasa?


Kubwa ya yote ni kwamba Sugu ameamua kuwapa zawadi maalumu mashabiki wake. Anakuja na albamu mpya! Ukisoma mahojiano haya mpaka mwisho utaweza kusikiliza single mpya kutoka kwake inayokwenda kwa jina Kambarage.
Ukitaka kujua zaidi mtu mzima Sugu kaongea sumu gani ingia bongocelebrity.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 09, 2009 | | Permalink |

Maoni: 1

  Tarehe July 14, 2009 3:01 AM Anonymous Anonymous Anasema:
MUONGO HUYU JAMAA MUASISI WA BONGO FLEVA NI SALEH JABIR CHINI YA DJ KIM. NA WIMBO WA ICE ICE BABY.
PIA KWENYE KUCHEZA ALIKUWEPO MUSSA SIMBA AU BLACK MOSES.HUYU JAMAA HAKUWEPO DSM KABISA.MUONGO


Idadi ya watu