728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, April 23, 2008

  tatiana kuwapa ari mpya wabunifu wa mavazi ?


  Mtendaji mkuu wa New Habari 2006 Ltd,Rosemary Mwakitwange akibadilishana mawazo na mshindi wa shindano la Big Brother Afrika II wa mwaka jana Tatiana Durao leo asubuhi walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari ndani ya hoteli ya movenpick

  Kutoka kulia ni mshindi wa shindano la Big Brother Afrika II wa mwaka jana Tatiana Durao, kati ni Mtendaji mkuu wa New Habari 2006 Ltd,Rosemary Mwakitwange pamoja na muwakilishi wa kinywaji cha redds,wakizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya hoteli ya Movenpick kuhusiana na maonesho yao mawili ya mavazi yatakayofanyika mjini Arusha na Dar

  Visura tano bora wa Tanzania wakiwa wamepozi kwa pamoja leo asubuhi ndani ya hoteli ya Movenpick wakati Tatiana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho yake mawilii ya mavazi,likianza lile la Arusha ambalo litakwenda sambamba na ufunguzi wa hoteli ya Naura prings,Hoteli Dada pamoja na zile za Ngurdoto na Impala

  Tatiana akiwasalimia waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya hoteli ya movenpick,kushoto ni Mtendaji mkuu wa New Habari 2006 Ltd,Rosemary Mwakitwange

  Mshindi wa shindano la Big Brother Afrika II wa mwaka jana Tatiana Durao kushoto akiwa amepozi na balozi wa kinywaji cha redds Victoria Martin leo asubuhi ndani ya hoteli ya Movenpick kabla ya kuongea na waandishi wa habari
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  7 comments:

  1. KWA HIYO NDO KESHAFIKA SIO???!!!

   ReplyDelete
  2. swali..

   ni tatiana ndio alishinda au ni richard sababu naona unaandika sana mshindi wa bba2

   ReplyDelete
  3. Dogo tunashukuru kwa picha, lakini wakati unamtambulisha huyu dada ni bora ukumbuke kuwa huyu alikuwa ni mshindi wa pili! Kwahiyo neno "mshindi wa pili" lazima uliweke na sio unaandika tu "mshindi wa big brother mwaka jana" Wewe dogo vipi lakini?!

   ReplyDelete
  4. WE BWANA!!! HUYO SI MSHINDI WA BIG BROTHER JAMANI, NAONA KILA MARA UNARUDIA UPUUZI HUO HUO, MSHINDI NI RICHARD, KWANI ULIKUWA WAPI WEWE WAKATI MSHINDI ANATAJWA!?? WABONGO BWANA KWA KUBABAIKA, MMEMVALISHA MPAKA BENDERA YA TANZANIA, KWANI YEYE MTANZANIA!!! UPUUZI MTUPU

   ReplyDelete
  5. Vipi wewe,mbona unasema mshindi was bb 11. kwani hujui alishinda richard? usitumislead. information yako lazima iwe na uhakika sio unalipua lipua tu..

   ReplyDelete
  6. LAbda ana sema mshindi akiwa anamaanisha wao ni kama kitu kimoja yaani aidhaa rich au tati wote ni washindi.Mambo ya familia hayo tena si unajua yaliyotokea jumbani BBA.....teh teh teh!

   ReplyDelete

  Item Reviewed: tatiana kuwapa ari mpya wabunifu wa mavazi ? Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top