Friday, June 29, 2007

Buriani Amina Chifupa


Amina Chifupa amezikwa jana na mamia ya watu, wakiwamo viongozi wa serikali, wananchi wa kawaida na wakazi wa kijiji cha Ihanjo,tarafa ya Lupembe, wilaya ya Njombe, mkoani Iringa
Picha kwa hisani ya Mpoki Bukuku wa gazeti la Mwananchi


Wengi aliwapa faraja na matumaini.


upendo wake haukuwa na mipaka.


hakupenda kujitenga, aliamua kujitoa hata kwa Wagonjwa


Utakumbukwa kwa mengi mpendwa wetu Amina Chifupa

Mbasha


Msanii wa muziki wa Injili Frola mbasha jukwaani akiimba kwa hisia, muziki wa Injili na wenyewe unalipa kwa sasa, kiasi hata kupelekea baadhi ya wasanii wa ubongo wa fleva kukimbilia huko, ukiwauliza kisa utaambiwa muziki wa injili una maslahi zaidi kuliko ubongo wa fleva.

asili


Baadhi ya densaz wa muziki wa asili kutoka kundi la Afrikali wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za asili.Muziki wetu wa asili umekuwa ukipuuzwa na kutopewa kipau mbele kuliko muziki wa Ubongo wa Fleva, huwezi amina hata ukienda kwenye maonesho ya muziki huo asilimia kubwa utakuta ni Wazungu tu, Sijui vya kwetu tutaanza kuvithamini lini,Hivi tatizo letu ni nini Wadau ? !

Thursday, June 28, 2007mastaa kibaoUmati wote huu ulibaki nje kutokana mahali hapo kutokuwa na nafasi ya kutosha, ama kwa hakika Amina alikuwa ni kipenzi cha wengi.mtangazaji wa kituo cha redio ya Clouds 88.4 FM Sebastian Ndege (mzee wa njia panda) akitangaza moja kwa moja kwenye msiba huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu.

Amina Chifupa alizaliwa mei 20,mwaka 1981.Alisoma shule ya msingi Ushindi mwaka 1988 hadi 1994 na baadaye shule ya sekondari Kisutu, Dar es Salaam mwaka 1995 mpaka 1998,kabla ya kuendelea katika shule ya sekondari ya Makongo kwa masomo ya kidato cha tano na sita, mwaka 1999 hadi 2001.

Mwaka 2001 alijiunga na masomo ya Uandishi wa habari katika chuo cha Uandishi wa habari Royal Dar es salaam na kuhitimu kwa kiwango cha stashahada mwaka 2003.Mbali ya hayo Amina Chifupa alikuwa ni moja ya watangazaji wa kwanza kuajiriwa na kituo cha redio ya Clouds 88.4 FM mwaka 1999, pia alifanikiwa kufungua kampuni yake binafsi ilioitwa kwa jina la Shughuli mwaka 2003.

kwa upande wa siasa Amina alianza safari yake kwa kuwa Kamanda wa tawi la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Mikocheni jijini Dar, alikuwa katibu wa kamati ya uchumi ya mkoa -UVCCM (Dar) mwaka 2004, kama vile haitoshi alikuwa mlezi wa UVCCM Bunju na Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mbagala Dar es salaam 2004 mpaka anafariki

Alipata Ubunge ,Desemba 28 mwaka 2005, akitakiwa kudumu katika Ubunge kwa miaka mitano hadi Desemba 27, mwaka 2010

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMINAMh Cheyo akihojiwa mara baada ya kufika msibani, Mh Cheyo ambaye pia ni mbunge alionesha simanzi na masikitiko makubwa kufutia kifo cha marehemu Amina Chifua

Wednesday, June 27, 2007

uso kwa uso


siku jarida la burudani la KITANGOMA lilipokutana uso kwa uso na Mh amina Chifupa, ambapo humo alieleza mambo yake mengi, zikiwemo ndoto zake za kufika mbali akiwa kama kijana

ucheshi na tabasamu


Mh Amina Chifupa alionesha ucheshi na tabasamu kwa kila mtu kama ambavyo anaonekana pichani, mstari wa nyuma wote ni watangazaji wenzake.Kushoto ni B 12,Gadna G Habash na wa mwisho kulia ni Sebastian Ndege mzee wa Njia Panda

Ujasiri Wake


Umakini na ujasiri wake katika kazi ulimletea mafanikio makubwa, ambayo kwa namna moja ama nyingine pia uliinua changamoto mpya ya kuongeza juhudi kwa kila jambo alilolifanya.Hapa alikuwa akipokea tuzo ya mtangazaji bora wa kike katika kituo cha Clouds 88.4 fm alipokuwa akifanyia kazi,Amina Chifupa aliwashinda watangazaji zaidi ya 30 wakati huo tuzo ziliandaliwa na kampuni ya George Inc

Nyota angavu iliozima Gizani


tupo katika wakati mgumu kwa sasa wa maombolezo kufuatia kifo chako. Hakika hekima zako, ucheshi na ukarimu wako, ujasiri wako na mengi mengineyo yatakumbukwa Daima.Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi mpendwa wetu..AMIN

wakati huo


Marehemu,Mh Amina Chifupa wakati wa uhai wake akiwa na mumewe Mohamed Mpakanjia kabla ya kutengana kwao

ametutoka.!


Mbunge wa viti maalum kupitia Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM), Amina Chifupa amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar

Tuesday, June 26, 2007

Kivyake.!


Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya zouk hapa nchini anayejulikana kwa jina la kisanii, Dee ameanza makamuzi kivyake.

Dee ambaye jina lake halisi ni Deo Mwanambilimbi, hapo awali alikuwa akiitumikia bendi ya Twanga Chipolopolo ameamua kuwa msanii wa kujitegemea baada ya kuenguliwa na bendi hiyo.

Pamoja na kuenguliwa huko, Dee amesema kuwa wala hato kata tamaa kuhusiana na suala la muziki, badala yake ataongeza juhudi zaidi kwa kujifanyia kazi zake binafsi za muziki.

Ili kulithibitisha hilo, Dee tayari amekwisha ikamilisha albamu yake ya kwanza ijulikanayo kwa jina la Uchona, ambayo iko sokoni na imekuwa ikifanya vizuri.

Kikubwa zaidi kutoka kwa mkali huyo wa zouk ameongeza kusema kuwa,pia yuko mbioni kuzikamilisha songi zake mbili ambazo anaamini pia zitakuwa moto wa kuotea mbali.

Dee, mpigaji kinanda makini na mwenye kipaji cha kuimba, amewahi kujitwalia tuzo ya mwanamuziki bora wa Zouk 2006 za Killimanjaro Music Awards ambazo hutolewa kila mwaka.

King


Msanii wa miondoko ya kizazi kipya, ajulikanaye kwa jina la king Lenny, hivi karibuni ametamka wazi kuwa ameokoka.King Lenny ambaye ameamu kubadili upepo na kuingia kwenye fani ya muziki wa Injili alisema kwa sasa anaachana na muziki wa kidunia na kuhamia kwenye mambo ya dini zaidi likiwemo na suala la kuokoka


Msanii huyo alikwisha ikamilisha albamu yake ya ubongo wa fleva ilioitwa Mashabiki iliyokuwa na jumla ya nyimbo saba na iko sokoni ikiendelea kuuzwa.

utamaduni


tamaduni na harusi zetu

Mie


Nami nilipata nafasi ya kuitembelea mbuga yetu ya Wanyama ya Ngorongoro

Big G na ubongo wa fleva

Hivi eti Wadau kwanini baadhi ya wasanii wa ubongo wa fleva muziki wao unafananishwa na BIG G ama babo gam

Binti machozi


Mwanamuziki wa kizazi kipya Judith Wambura ambaye anafahamika kwa majina mengi likiwemo la Lad J Dee, Jide,Binti Machozi,Komando,Mama some food na mengineyo kwa sasa anatamba na singo yake ya siku hazigandi.
Msanii huyu amejipatia sifa, heshima na mafanikio makubwa kwani kwa sasa anamiliki bendi yake ya Machozi Band na pia amefungua studio ya kurekodia muziki inayoitwa JAG RECORDS ambapo baadhi ya wasanii tayari wamekwishaanza kurekodi kazi zao.

,

Monday, June 25, 2007

kubwa kuliko


Mtangazaji mahiri wa Clods 88.4 Hamis Mandi ambaye anatangaza kipindi cha XXL a.k.a Kubwa Kuliko amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na juhudi ya kazi yake ya utangazaji kiasi hata ya kupachikwa majina lukuki likiwemo la B 12, B Dozen, Mzee wa kubwa kuliko, Kubwa zaidi kwa sasa anatambulika kama balozi wa Kinywaji cha Red Bull

Saturday, June 23, 2007

Mlima Kolero


Baadhi ya waigizaji wa filamu mpya ya Mlima Kolero wakiwa katika maandalizi, mlima huo inaelezwa kuwa una historia kubwa kwa wakazi wa mji kasoro bahari yaani Morogoro, inasemekana kuwa mlima huo mpaka sasa una miujiza mingi tu

Thursday, June 21, 2007

Langa


Msanii wa kizazi kipya (ubongo-wa fleva) mwenye nyeusi akiwa na baadhi ya

wasanii wenzake jukwaani.Langa amekiri wazi kuwa hata kubali kuyumbishwa juu ya muziki wa hip hop kwani ndio muziki anaoukubali zaidi kuliko muziki wowote.!

Wednesday, June 13, 2007

Mchovu


kazi ipo ndani ya ubongo wa fleva

Kidole


Gea Habib ambaye pia ni moja ya watangazaji machachari wa Clouds 88.4 fm

Tuesday, June 12, 2007

Hee.!


Wanne Star akionesha umahiri wake wa kucheza na nyoka,kutokana na fani hiyo wanne amekuwa akikimbiwa na warembo kibao aliowatokea, na pia yeye binafsi amedai kuwa imemletea matatizo katika suala zima la kiimani, kwa sasa yeye anadai hana dini.!

Bongo


Bongo yetu haina noma wala nini imejaaliwa warembo wa kila aina

Inauzwa


Mama Salma Kikwete akiinadi albamu ya nyimbo za injili ya Haleluya iliyozinduliwa hivi karibuni ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuliwa na umati mkubwa wa watu

hisia


Msanii wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Upendo Nkone,akiimba wimbo wa "Mungu Baba" kwa hisia.! Msanii huyu nae amejipatia sifa na hasa kwa kuimba nyimbo zake nyingi kwa hisia kiasi hata ya kuziteka hisia za watazamaji wakati wa maonesho yake.

Thursday, June 7, 2007

studio


Jah-Rule akiwa ndani ya studio za Clouds 88.4 fm akirekodi jingo mara alipotua bongo, kiukweli jamaa hakujivunga kujiachia

Mrithi


Dina Marios akitangaza kipindi cha Leo tena ambacho hapo awali Mh Amina Chifupa alikuwa akitangaza ndani ya Clouds 88.4 fm

vazi


Modo akionesha vazi lililobuniwa na mchora katuni maarufu bongo Masoud Kipanya a.k.a Kipanya

hapatoshi


Siku Mr nice alipojikuta mwenye wakati mgumu mikononi mwa polisi

tulii


Msanii wa bongofleva Ray C akiwa amepozi na mkali wa hip hop Jah Rule alipotua bongo kwa onesho maalum ndani ya tamasha la fiesta mwaka jana

 
Nafasi Ya Matangazo